MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda jana alifanya ziara ya kukagua
barabara ya Mwanayama 'A' hadi Makumbusho ambayo imeharibika kutokana na
mvua zinazoendelea kunyesha.
Akizungumza
baada ya kukagua barabara hizo alisema amewapa watendaji wa manispaa ya
Kinondoni wiki mbili kushughulikia tatizo hilo kutokana na adha ya
magari yanayotumia barabara hiyo.
"Sasa
nimeiagiza Manispaa, nimewapa wiki mbili kuhakikisha mashimo yote yawe
yamezibwa, na wakishindwa nitawasaidia kuwawajibisha na kuchukua hatua
stahiki." Alisema Paul Makonda
Alisema kuwa kuharibika kwa barabara nyingi katika manispaa hiyo ni kutokana na kujengwa chini ya kiwango.
Makonda
alisema fedha zinatolewa kwa ajili ya ujenzi lakini baadhi ya watendaji
wanajenga chini ya kiwango na kuwapa adhabu wananchi wanaotumia
barabara hiyo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment