
Katika Kipindi cha miezi nane
kuanzia Julai 2015 hadi Februari mwaka huu, Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA) imekusanya jumla ya Sh Trilioni 8,569,854.40 ikilinganishwa na
lengo la kukusanya Sh trilioni 8,685,991.52 ambayo ni sawa na asilimia
99 ya makusanyo yote.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Kamishna
Mkuu wa Mamlaka hiyo, Alphayo Kidata wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu mwenendo wa ukusanyaji wa mapato, matumizi ya mashine za
EFDs, kusitisha kwa bei elekezi na usajili wa vyombo vya moto.
Amesema lengo la Mamkala hiyo ni
kukusanya Trilioni 12.3 hadi ifikapo Juni mwaka huu na kwamba asilimia
moja iliyobakia katika kukamilisha asilimia 100 ya ukusanyaji wa mapato
kati ya Julai mwaka jana hadi Juni mwaka huu, itakamilika ndani ya
miezi nne iliyosalia ambayo itaisha Juni mwaka huu.
Amesema pia kwa mwezi Februai pekee, Mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya mapato ya kiasi cha Sh Trilioni 1,040,540.20 kwa
upande wa Tanzania Bara na Zanziba ambayo kiasi hicho ni sawa na
asilimia 101.18 ya lengo la ukusanyaji ambayo ilikuwa ni Sh Trilioni
1,028,379.40 kwa mwezi.
Amesema kuongezeka kwa mapato haya
kunatokana na kudhibiti kwa mianya ya ukwepaji wa kodi na kuweka
mazingira rafiki kwa mlipa kodi, kurekebishwa kwa misamaha ya kodi
ambayo ilikuwa inachangia upotevu wa mapato, kuongezeka kwa watumiaji wa
mashine za EFDs pamoja kudhibiti eneo la forodha ambalo lilikuwa
linasababisha upotevu wa mapato ya TRA.
Maeneo yaliyochangia kuongezeka kwa mapato hayo:
“Maeneo ambayo yamechangia
kuongezeka wa mapato haya ni kuimarishwa kwa bandari yetu kwa kuziba
mianya ya ukwepaji kodi , kurekebishwa kwa misamaha ya kodi ambayo hapo
awali ilikuwa inachangia upotevu wa ukusanyaji wa mapato, kuongezeka kwa
matumizi ya utumiaji wa mashine za EFDs kwa wafanyabiashara, Mamlaka
kuwatengenezea mazingira mazuri kwa walipa kodi, kudhibitiwa kwa eneo la
forodha ambapo wajanja wachache walikuwa wanatumia mwanya huu
kuikosesha serikali mapato” amesema Kidata.
Kwa mwezi Januari walikusanya Trilioni 1,079,993.20:
Katika kipindi cha Januari pekee,
Mmalaka hiyo ilikusanya kiasi cha Trilioni 1,079,993.20 kwa Tanzania
bara na visiwani ambapo kiasi hicho ni sawa na asilimia 102 ya lengo la
Sh Trilioni 1,059,864.00 kwa mwezi.
“Makusanyo haya ya Januari
yametokana na ari na uthubutu ambao TRA imejiwekea katika kusimamia na
kuhakikisha inaendelea kuziba mianya ya ukwepaji kodi na kuweka
mazingira rafiki kwa mlipakodi kwa kulipa kwa wakati na urahisi kwa
kutumia mifumo mbalimbali iliyopo”ameongeza.
Faini ya mashine za EFDs kwa Wafanyabaishara:
Kidata amesema katika kipindi cha
mwezi Februari pekee, Mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya faini ya Sh
800milioni kwa watu wa jiji la Dar es Salaam ambapo walikiuka na kufanya
makosa katika utumiaji wa mashine za EFDs.
“Kuanzia mwezi Machi mwaka huu kila
mtu anayetakiwa kutumia mashine za EFDs atumie vinginevyo hatua kali
za kisheria zitafuatwa”amesema Kidata.
Amesema utaratibu wa matumizi ya EFDs
ulifanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza iliwahusisha
wafanyabiashara ambao wamesajiliwa kutoa VAT na awamu ya pili
ilihusisha wafanyabaishara ambao hawakusajiliwa na Vat ambao mauzo yao
kwa mwaka ni zaidi ya Sh 14milioni.
Serikali kugawa bure mashine za EFDs:
Kwa upande wake Kamishna wa Kodi za
Ndani kutoka TRA, Yusuph Salum alisema serikali imeagiza Mamlaka ya
Mapato nchini kutoa bure mashine za EFDs kwa wafanyabiashara wadogo
ambao uwezo wa kununua mashine hizo unaweza kuathiri mitaji yao ya
biashara.
“Kwa sasa tuko katika hatua za
mwisho kukamilisha manunuzi wa mashine za uniti 5700 na kwamba
wafanyabiashara wakubwa hawatahusika na mgao wa mashine hizi za bure
bali wao wataendelea na utaratibu wa zamani wa kujirejeshea gharama za
mashine kupitia ritani za mwezi” amesema Salum.
Amesema pamoja na kuwepo kwa sheria
inayomtaka mfanyabiashara kununua , kutumia mashine, kutoa risiti na
kulipa kodi, TRA imebaini wafanyabiashara waliowengi hawana mashine hizo
za kutolea risiti pindi wanapofaya mauzona hivyo kuikosesha serikali.
Usajili wa magari:
Kidata alisema TRA, imefanya ukaguzi
na kubaini kuwepo kwa magari ambayo yaliingizwa nchini na kusajiliwa
bila kufuata taratibu za forodha hivyo kuyafanya yamilikiwe bila
kulipiwa kodi stahiki na kwamba kuna jumla ya magari 9000 ambayo
yanaingia nchini na kutolewa.
“Wamiliki wa magari wote tayari
tumeshawataarifu kufika TRA kufanyiwa uhakiki ili kuyalipia kodi
stahiki lakini pia kumekuwa na matumizi mabaya ya misamaha iliyotolewa
hasa kwa upande wa magari, hivyo utaratibu wa misamaha uliwekwa kwa
ajili ya kuwapa nafuu wawekezaji ili wahusika wamekuwa wakiitumia vibaya
kwani magari yameingizwa mengi kuliko mahitaji na kupelekea serikali
kukosa mapato” amesema
Amesema sheria za kodi zinatoa
misamaha mbalimbali kupitia utaratibu wa Kituo cha Uwekezaji cha
Taifa(TIC) na mashirika yasiyo ya kiserikali na kwmaba nia na madhumuni
ya misamaha hiyo ni kuvutia uwekezaji na kutoa unafuu wa huduma kwa
jamii.
Kufutwa kwa bei elekezi:
Katika hatua nyingine, Mamlaka hiyo
imefuta bei elekezi katika mchakato wa uthaminishaji wa bidhaa
bandarini kwa sababu ni kinyume cha sheria ya Jumuiay ya Afrika
Mashariki na kwamba TRA itaendesha shughuli za kiforodha kulingana na
sheria husika.
“Tumeona bei elekezi haisaidi kwa
sababu uingizaji wa bidhaa unatawaliwa na sheria ya Afrika Mashariki
ambapo na sisi Tanzania ni wanachama, hivyo Mamlaka itadhibiti ukaguzi
na uthaminishaji halisi ili kila mfanyabaishara alipe ushuru na kodi
kulingana na thamani ya bidhaa husika, hata hivyo uthaminishaji mizigo
kwa wafanyabiashara umepelekea wengine kulipa kodi kubwa kuliko thamani
ya bidhaa husika” amesema.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment