Rais MAGUFULI Atoa Zawadi Ya Pasaka Ya Milion 9 Kwa Watoto Yatima na Wazee Wasiojiweza

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ametoa zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni tisa laki tatu na elfu sabini kwa vituo 24 vya kulelea watoto yatima na wazee wasiojiweza nchini kwa lengo la kuungana nao katika kusheherekea sikukuu ya Pasaka.

Msaada huo uliotolewa na Rais ni pamoja na Mchele, Mbuzi na mafuta ya kupikia ambao utakwenda kwenye vituo 6 vya watoto yatima vilivyoko jijini jijini Dar es salaa, na vituo viwili vya Zanzibar, Tabora, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Kagera na Morogoro na kituo kimoja kwa mikoa ya Tanga, Ruvuma, Shinyanga, Mtwara na Mara.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Rais kwa wafanyakazi wa vituo hivyo Kamishna wa Ustawi wa Jamii Rabikila Mushi amesema kuwa msaada huo uliotolewa na Rais Magufuli ni moja ya utaratibu wa kawaida wa Marais tangu awamu nne zilizopita kuwapatia zawadi makundi maalum vyakula ili kuwawewezesha kufurahi na kusherehekea sikukuu mbalimbali kama wananchi wengine wa kawaida katika jamii.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment