Ajali Mbaya Yaua 25 Singida... Ni Baada ya Mabasi Mawili Kugongana!

Watu 25 wamefariki dunia, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya mabasi mawili kugongana huko wilayani Manyoni mkoani Singida.
Mabasi hayo yanayomilikiwa na Kampuni ya City Boy, moja lilikuwa linasafiri kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Kahama na lingine lilikuwa linatoka Kahama kwenda Dar es Salaam.

Akizungumzia ajali hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Thobias Sedoyeka amesema idadi ya majeruhi bado haijajulikana japo kuwa amesema ni wengi.
“Ni kweli ajali imetokea Manyoni na tupo eneo la tukio tunaendelea na utaratibu wa kuondoa majeruhi na miili pamoja na mabasi haya barabarani,” amesema Kamanda Sedoyeka.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment