Kauli ya SIMBA SC Kuhusu Golikipa Wao Kufungiwa Miaka 10 Kucheza Soka na TFF

Bado headlines za uongozi wa klabu ya Simba kuendelea kueleza hisia zao za kutofurahishwa na shirikisho la soka Tanzania TFF na bodi ya Ligi jinsi wanavyopanga ratiba ya Ligi Kuu Tanzania bara na kuibadili kila siku, mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara ameongea jipya. 

Manara anaamini na anaomba ili haki itendeke ni bora TAKUKURU wakachunguze masuala ya rushwa kwa tuhuma za upangaji wa matokeo ya mechi za Ligi daraja la kwanza, ambazo zinaigusa klabu yao kutokana na golikipa wao Denis Richard aliyekuwa kwa mkopo Geita Gold kufungiwa miaka 10 na kupigwa faini milioni 10.  

Manara anaamini na anaomba ili haki itendeke ni bora TAKUKURU wakachunguze masuala ya rushwa kwa tuhuma za upangaji wa matokeo ya mechi za Ligi daraja la kwanza, ambazo zinaigusa klabu yao kutokana na golikipa wao Denis Richard aliyekuwa kwa mkopo Geita Gold kufungiwa miaka 10 na kupigwa faini.
Haji Manara
“Ni kweli Denis kafungiwa miaka 10 lakini sisi kama Simba ili tuseme kitu ni lazima TAKUKURU wafanye uchunguzi haki itendeke halafu ndio tutatoa tamko, ila kwa sasa hatuwezi kusema tunafanyaje hili jambo kuna tuhuma za rushwa kama atakuwa kweli kahusika na upangaji wa matokeo Simba haiwezi kutetea jambo hilo” >>> Haji Manara 

Kama utakuwa unakumbuka vizuri TFF kupitia kwa kamati yake ya maadili April 3 2016 ilitangaza kuwafungia baadhi ya viongozi na wachezaji waliobainika kujihusisha na tuhuma za upangaji wa matokeo katika mehi za Ligi daraja la kwanza iliyokuwa inahusisha michezo ya Kundi C, golikipa Denis Richard alitajwa kuhusika.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment