MGAHAWA mmoja uliopo ndani ya jengo la
ghorofa sita lililopo mtaa wa Lumumba mkabala na Mahakama ya Wilaya ya
Ilala jijini Dar es Salaam, umenusurika kuungua baada ya kutokea
hitilafu ya umeme iliyodaiwa chanzo chake ni waya wa friji ulioshika
cheche za moto na kuwaka.
Akizungumza na mwanahabari wa mtandao huu, mmiliki wa jengo hilo,
Hussein Said alisema hitilafu hiyo ilianzia katika chumba cha mgahawa
kilichopo chini na hakuna aliyejeruhiwa zaidi ya kuungua kwa baadhi ya
viti na vyombo.
Alisema kikosi cha zimamoto kilifika eneo la tukio kwa muda muafaka na
kuuzima moto huo usisambae wala kuleta athari nyingine yoyote
Na Denis Mtima/Gpl
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment