Akizungumza katika Uzinduzi wa Baraza la tisa la Wawakilishi la Zanzibar Rais Dkt. Shein amesema kwa mujibu wa Katiba aliamua kumteua balozi Seif Ali Idd kuwa makamu wa pili wa rais ili kuunda serikali visiwani humo kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.
Dkt. Shein amewahakikishia wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwa serikali atakayoiunda itasimamia misingi ya haki, uwajibikaji,haki, uwazi na usawa wa wananchi wote bila kujali itikadi zao.
Aidha Dkt. Shein amesema kuwa katika kipindi atakachokaa madarakani ataendelea kuulinda Muungano wa serikali mbili wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa tangu mwaka 1964.
Dkt. Shein ameongeza kuwa atahikikisha serikali hizo mbili zinafanya kazi kwa umoja na ukaribu zaidi katika kupanga na kutekeleza mikakati ya kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.
Aidha amesema kuwa kwa kushirikiana na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema watadumisha Umoja na amani iliyopo visiwani humo huku akikisitiza kuwa maneno yanayotolewa na wapinzani hayamnyimi usingizi.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment