Ndege hiyo yenye namba MS181 aina ya airbus A320 iliyokuwa imewabeba abiria 81 kutoka Alexandria kuelekea Cairo ilitekwa nyara baada ya abiria mmoja kusema amevaa mkanda wa mabomu ya kujitolea mhanga.
Shirika la ndege hiyo limesema kuwa majadiliano yamesababisha kuwachiwa huru kwa abiria wote waliokuwa ndani isipokuwa wafanyakazi wa ndege hiyo na abiria wanne wa kigeni.
Kanda ya video iliochukuliwa imeonyesha watu wakiondoka katika ndege hiyo na kupanda basi.
Uwanja wa ndege wa Larnaca umefungwa huku ndege zilizokuwa zikisubiriwa kutua zikielekezwa kwingineko.
Rubani anasema kuwa abiria mmoja alimwambia kuwa amevaa nguo ya ndani iliyojaa vilipuzi na kuilazimisha ndege hiyo kutua katika uwanja wa ndege wa Larnace, kulingana na taarifa ya wizara ya uchunkuzi wa angani nchini humo.
”Habari tulionayo kufikia sasa ni kwamba mtekaji huyo ni mmoja, mtu huyo hajataka chochote”, ofisa wa wizara ya masuala ya kigeni nchini humo Alexandros Zenon aliiambia runinga ya Ufaransa.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment