DR. SHEIN Alivyoapishwa Rasmi Kuwa Rais wa Awamu ya 7 wa Zanzibar Leo

Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein ameapa kuwa Rais kwa mujibu wa katiba katika kuongoza wananchi wa Zanzibar kwa muda wa miaka 5.

Rais Mteule ameapishwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Jaji Omary Othman Makungu mbele ya viongozi wa nchi pamoja na viongozi wa dini na kushuhudiwa na mamia ya wananchi katika uwanja wa Amani mjini Unguja.

Baada ya Rais Shein kuapishwa viongozi wa dini wameomba dua wakiongozwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis na kufuatiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Mhashamu Augustino Shayo na Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Zanzibar Padre Michael Henry Hafidh.

Viongozi mbalimbali wamehudhuria Kiapo hicho akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, viongozi wastaafu wa kitaifa na mamia ya wananchi.

Aidha Rais Dkt. Ali Mohamed Shein ameapishwa na kuwa Rais wa awamu ya saba kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na kukagua gwaride rasmi, pamoja na itifaki nyingine kufuatia.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment