Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewateua ndugu Ritha Enespher Kabati na ndugu Oliver Daniel Semuguruka wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) na ndugu
Lucy Fidelis Owenya
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa Wabunge Wanawake wa viti
Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ikumbukwe kuwa Tume katika Kikao chake cha tarehe
11/11/2015 ilifanya Uteuzi wa Wabunge Wanawake wa Viti Maalum 113 kwa mwaka
2015. Hata hivyo, Wabunge Wanawake wa Viti Maalum walioteuliwa jumla yake
ilikuwa ni 110 kati ya 113 ambapo Viti vitatu (3) vilibakizwa kusubiri Uchaguzi
wa Majimbo nane (8) ambayo Uchaguzi wake ulihairishwa kutokana na sababu
mbalimbali.
Uteuzi wa awali ulihusisha Vyama vitatu vilivyofikisha
asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Wabunge kama matakwa ya Katiba
yanavyotaka. Vyama vilivyopata asilimia
tano ambayo ilikuwa 780,226 ni.
Na.
|
Jina
la Chama
|
Idadi
ya Kura baada ya majimbo 256 kufanya Uchaguzi wa Wabunge
|
1.
|
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
|
8,332,953
|
2.
|
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
|
4,627,923
|
3.
|
Chama cha Wananchi (CUF)
|
1,257,051
|
Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa Majimbo hayo nane
(8), Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama
cha Wananchi (CUF) ndivyo vilivyoendelea kupata angalau asilimia tano (5%) ya
Kura zote halali za Ubunge, kwa maana hiyo, vyama hivyo ndivyo vitaendelea kuhusishwa
kwenye Mchakato wa kugawanywa hivyo Viti 3 vilivyobaki.
IDADI YA KURA ZA
CCM, CHADEMA NA CUF BAADA YA UCHAGUZI WA MAJIMBO NANE (8) KUKAMILIKA
Baada ya kukamilika Uchaguzi katika majimbo nane (8)
Idadi ya Kura kwa Vyama vya CCM, CHADEMA na CUF ni kama ifuatavyo:
Na.
|
Jina la Chama
|
Idadi ya Kura baada ya
majimbo 256 kufanya Uchaguzi wa Wabunge
|
Idadi ya Kura baada ya
Uchaguzi wa Majimbo nane (8) kukamilika
|
Jumla ya Kura zote halali za
Ubunge.
|
1.
|
Chama
Cha Mapinduzi (CCM)
|
8,332,953
|
162,535
|
8,495,488
|
2.
|
Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
|
4,627,923
|
92,958
|
4,720, 881
|
3.
|
Chama
cha Wananchi (CUF)
|
1,257,051
|
17,860
|
1,274,911
|
1.0.
MGAWANYO
WA VITI VITATU (3) VYA WABUNGE WA VITI MAALUM
Kukamilika kwa Uchaguzi wa majimbo nane (8) kumeonesha
kuwa, Viti vitatu vilivyosalia vitagawanywa kwenye vyama viwili vya CCM na
CHADEMA kwa mpangilio ufuatao:
CHAM A CHA
MAPINDUZI (CCM)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha
Mapinduzi ni 8,495,488. Hivyo ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CCM:
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ambazo CCM kimepata
unazidisha kwa Idadi ya Viti Maalum vyote na kugawanya kwa Idadi ya Kura halali
za Ubunge kwa vyama vilivyopata angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za
Ubunge. Hivyo,
8,495,488 X 113
|
=
66.24 ambayo ni 66
|
14,491,280
|
Hivyo, CCM watakuwa na Viti 66 vya Wabunge wa Viti
Maalum, awali walikuwa na viti 64.
CHAMA CHA WANANCHI
(CUF)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha
Wananchi (CUF) ni 1,274,911. Hivyo
ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CUF:
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ambazo CUF kimepata
unazidisha kwa Idadi ya Viti Maalum vyote na kugawanya kwa Idadi ya Kura halali
za Ubunge kwa vyama vilivyopata angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za
Ubunge. Hivyo,
1,274,911
X 113
|
= 9.9
ambayo ni 10
|
14,491,280
|
Hivyo, CUF wataendelea kubakia na Viti 10 kwa kuwa
katika Chaguzi za Majimbo nane (8) hawakuweza kuongeza Kura ambazo
zingewaongezea Idadi ya Wabunge wa Viti Maalum.
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni 4,720,
881. Hivyo ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CHADEMA:
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ambazo CHADEMA kimepata
unazidisha kwa Idadi ya Viti Maalum vyote na kugawanya kwa Idadi ya Kura halali
za Ubunge kwa vyama vilivyopata angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za
Ubunge. Hivyo,
4,720,881 X 113
|
=
36.81 ambayo ni 37
|
14,491,280
|
Hivyo, CHADEMA watakuwa na Viti 37 vya Wabunge wa Viti
Maalum, awali walikuwa na viti 36.
CHAMA CHA WANANCHI
(CUF)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha
Wananchi (CUF) ni 1,274,911. Hivyo
ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CUF:
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ambazo CUF kimepata
unazidisha kwa Idadi ya Viti Maalum vyote na kugawanya kwa Idadi ya Kura halali
za Ubunge kwa vyama vilivyopata angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za
Ubunge. Hivyo,
1,274,911
X 113
|
= 9.9
ambayo ni 10
|
14,491,280
|
Hivyo, CUF wataendelea kubakia na Viti 10 kwa kuwa
katika Chaguzi za Majimbo nane (8) hawakuweza kuongeza Kura ambazo
zingewaongezea Idadi ya Wabunge wa Viti Maalum.
MAPENDEKEZO YA
MAJINA YA UTEUZI WA VITI MAALUM KWA VYAMA VYA CCM NA CHADEMA
Tume hufanya uteuzi kwa kufuata mtiririko wa orodha iliyowasilishwa
na Katibu wa Chama husika, kwa mantiki hiyo Tume imewateua Wabunge hao kama
ilivyojitokeza katika orodha za Vyama vya CCM na CHADEMA.
Katika orodha
iliyowasilishwa na CCM majina nambari 65 naa 66 ni
65.
Ndugu Ritha Enespher Kabati
66.Ndugu Oliver Daniel Semuguruka.
Katika Orodha iliyowasilishwa na CHADEMA jina nambari
37 ni
37. Ndugu
Lucy Fidelis Owenya.
Asanteni kwa
kunisikiliza,
Jaji Mst Mh. Damian Z. Lubuva
MWENYEKITI
WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment