Maafisa wa Kenya, Akiwemo Katibu Mkuu wa Nishati Wadakwa Bandari ya Tanga!



Maafisa kadhaa wa Kenya wakiwemo Katibu mkuu wa wizara ya nishati wameshikiliwa na maafisa wa uhamiaji mjini Tanga baada ya kujiingiza kwa siri katika msafara wa Waziri wa nishati wa Uganda aliyekuja nchini kufanya mazungumzo "ya siri" na serikali ya Tanzania kuhusu sakata la bomba la mafuta.

Wamenyang'anywa pasport na kuwekwa kizuizini mpaka mazungumzo yatakapoisha ndipo waruhusiwe kuuliza feedback ya kikao.

Jana Waziri wa nishati wa Uganda alikuja kufanya mazungumzo na serikali ya Tanzania kumbe jamaa walikua wamejichomeka kisiri na kujifanya nao ni Waganda, walipofika tu wakastukia wamefanyiwa umafia kwa kuzungukwa pande zote na kunyang'anywa passport zao.

Mashuhuda wanadai jamaa walibaki kulia lia tu wakaambiwa kaeni hapa mpaka tutakapo maliza mazungumzo ndipo mrudi kwenu, mpaka mida hii Waziri wa Uganda yupo kwenye mazungumzo na haijulikani hatma ya maafisa hao wa Kenya.

Naona Magufuli sasa anaanza kurudisha hadhi ya Tanzania, ule unyang'au nyang'au tuliokukwa tunafanyiwa na hawa waji
nga sasa utakwisha.
UPDATES: Maafisa hao wameshaachiwa
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment