Tukio hilo la kusisimua lilitokea dakika ya 86 ya mchezo huo wa Panama dhidi ya Veyula wakati huo timu ya Veyula ikiongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Panama na kama unavyojua presha inavyokuwa pindi timu inapokuwa nyuma kutafuta bao la kusawazisha dakika za majeruhi.
Picha lilianza baada ya mchezaji mmoja wa Veyula kuumia ndani ya uwanja na kukaa muda mrefu akiugulia maumivu bila kutolewa nje kama kanuni zinavyotaka basi bahna kocha wa Panama Salum Dunia akaanza kumhoji kwa jazba mwamuzi wa mezani Peter Mdachi ambaye hakuonyesha ushirikiano mzuri kwa kocha huyo na wakati wakiendelea kuzozana mwamuzi huyo alimwita mwamuzi wa kati Bryson Msuya ambaye alimlamba nyekundu kocha huyo.
Kuamrishwa huko kutoka nje kulimzidishia zaidi hasira kocha Dunia ambaye bila ajizi alimchapa kofi zito mwamuzi Peter Mdachi na kuamsha vurumai uwanjani hapo kwa timu zote mbili kabla ya hali kutulia na kumalizia dakika chache zilizosalia na hatimaye Veyula kuibuka na ushindi mwembamba wa bao hilo moja lililofungwa na Gervas John kipindi cha kwanza.
Mwendelezo wa ligi hiyo katika dimba la Jamhuri Dodoma ilishuhudiwa Area C wakiendelea kutikisa hatua ya sita bora kwa kuibuka na ushindi mnono wa bao 3-0 dhidi ya Kanda ya kati kupitia mabao mawili ya Salum Ngadu dakika za 14,76 na Mohamed Idd dakika ya 36 na kujiweka katika mazingira mazuri ya kuwa mabingwa wapya wa mkoa wa Dodoma.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment