SAMATTA Anacheza Soka Ubelgiji, Hivi ni Viwango Vya Mishahara Vya Wachezaji wa Ligi Hiyo

Najua unatamani kujua maisha ya wanasoka wa Ubelgiji hususani katika kipindi hiki anachocheza soka mtanzania Mbwana Samatta nchini humo, kiukweli mshahara wa Samatta haupo wazi katika vyombo vya habari, ila Ligi ya Ubelgiji wachezaji wanalipwa kwa mwezi.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.xpats.com hadi kufikia April 10 2015 mishahara ya wachezaji wengi wa Ligi Kuu Ubelgiji ilikuwa inatajwa kuwa ya wastani wa euro 253,586 kwa mwaka ambazo ni zaidi ya milioni 600 za kitanzania kabla ya kukatwa kodi pamoja na bima.
Samatta-3
Kwa mwezi huwa inatajwa kufikia wastani wa euro 20000 ambazo ni zaidi ya milioni 45 za kitanzania. Klabu ya Anderlecht iliyopo nafasi ya tatu katika Ligi, ndio inatajwa kuwa klabu inayolipa mishahara mikubwa zaidi, kwa mwaka Anderlecht inalipa hadi  euro 600000 ambazo ni zaidi ya bilioni 1.4 za kitanzania kwa mchezaji mmoja.
Klabu ya KRC Genk anayocheza nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta inatajwa kuwa miongoni mwa vilabu tajiri ndani ya Ligi Kuu Ubelgiji, ila kwa mujibu wa www.xpats.com, wachezaji wengi wao Ubelgiji hulipwa kati ya euro 25000 hadi 50000 kwa mwezi.
CHANZO CHA STORI: www.xpats.com
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment