Meneja Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray (kushoto) akitoa
taarifa yake kwa wanahabari (hawapo pichani).Kulia ni Ofisa habari wa
Idara ya Habari Maelezo,Frank Mvungi.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.
Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA) ikishirikiana na Jeshi la Polisi nchini imekuwa ikibaini baadhi ya madereva wanaokiuka Masharti ya leseni ya Kusafirisha abiria na wengine kutokuwa na leseni ndio maana wameona kuchukua hatua hiyo ya kukamata na kuwapeleka mahakamani madereva na Makondakta wanao kiuka masharti ya leseni zao. Pia amewaasa wamiliki wa mabasi na wafanyakazi wakiwemo madereva na Makondakta wa mabasi ya Daladala kuzingatia masharti ya Leseni za usafirishaji wanapotoa huduma ya usafirishaji kwa umma na wananchi kwa ujumla wamewaomba kutoa ushirikiano pale ambapo wanaona madereva wanakiuka masharti ya reseni za usafirishaji, kuongeza nauli, kukatisha njia au kutumia njia ambayo haijapangwa na Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA).
Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA), David Mziray akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na kukamatwa kwa mabasi yanayobainika kuvunja Masharti ya Reseni nyakati za asubuhi na jioni jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa mabasi 36 yameshakamatwa na kesi zao zipo mahakama ya Kinondoni na Ilala jijini Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA), David Mziray akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kulia ni Afisa habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Frenk Mvungi.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment