Augustino MREMA Aongea Kwa Mara ya Kwanza Toka Kesi na James MBATIA Imalizwe… Zile Milioni 40 Je? [+VIDEO]

Mahakama kuu kanda ya Moshi Kilimanjaro imeridhia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Mbunge wa Vunjo James Mbatia (NCCR) na aliyekua mbunge wa jimbo hilo Agustino Mrema hivyo Mahakama chini ya jaji anayekua anasikiliza kesi hiyo Lugano Mwandambo iliridhia shauri hilo kuisha na kwamba James Mbatia ndiye Mbunge halali wa Vunjo na Mrema atatakiwa kulipa sehemu ya gharama za mawakili wa Mbatia shilingi Milioni 40 kabla ya June 6 2016.

Siku huu uamuzi unatangazwa April 4 2016 Augustino Mrema hakuwepo Mahakamani na baada ya millardayo.com na AyoTV kumpata April 5 2016 akasema yafuatayo >>> ‘Sikuhudhuria Mahakamani sababu nilishakubaliana na Wakili wangu kwamba ningeweza kubaki kufanya kazi nyingine nyumbani‘

‘Kitu Watanzania wasichoelewa ni kwamba maelewano niliyoafikiana na Mbatia sio kweli kwamba niliondoa hiyo kesi Mahakamani, kama ningetaka kufanya hivyo sikuwa na sababu ya kutafuta maelewano na Mbatia, sisi tulifika mahali tukakubaliana na Mbatia kwa manufaa ya Wananchi wa Vunjo tuiondoe hiyo kesi na aliyenihamasisha mpaka nikaondoa kesi ni James Mbatia mwenyewe‘ – Mrema

Kwenye sentensi nyingine Mrema amesema ‘kesi zina gharama kubwa na katika huu muda mfupi tu kesi ilivyokua Mahakamani gharama zilizokwishatumika ni kubwa na tumekubaliana kusaidiana na James Mbatia, ni hela nyingi watu wanashangaa lakini jiulize kama hii kesi tungeiendeleza tu kwa ubabe ingekuaje‘

‘Madai ya labda milioni 200 au 150 ningedaiwa ningetoa wapi? maana hiyo ni kuja kuuza rasilimali nyumba zangu Kilaracha, Dodoma au Njia Panda… kwahiyo tumeiondoa kwa manufaa yetu, nimekubali yaishe na kumtambua James Mbatia kama Mbunge wangu‘ – Mrema
Kuyapata yote aliyosema Mrema kuhusu hii ishu bonyeza play hapa chini
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment