Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad kesho
ataelezea mwelekeo wake kisiasa, ikiwamo kufafanua kiundani uamuzi wa
chama hicho kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.
Mgombea
huyo wa urais Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana
ataeleza mambo hayo ikiwa imepita takribani wiki moja tangu Baraza Kuu
la chama hicho kutoa msimamo wake wa kutomtambua Rais wa Zanzibar, Dk
Ali Mohamed Shein pamoja na wawakilishi na madiwani.
CUF
kilisusia kushiriki uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu
baada ya Oktoba 28 mwaka jana, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya urais, uwakilishi na udiwani,
akisema kulikuwapo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.
Habari
kutoka ndani ya chama hicho zinaarifu kuwa mkutano wa kiongozi huyo
utakuwa wa kwanza kwake, tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio na
ataeleza mambo muhimu yatakayotoa picha halisi ya mwelekeo wake na CUF.
“Katika
mkutano uliopita tamko lilikuwa la Baraza Kuu ila keshokutwa (kesho)
Maalim Seif atazungumza kama Katibu Mkuu na aliyekuwa mgombea urais.
Kuna masuala mengi atayaeleza kwa kina, hasa hili la uamuzi wa CUF
kususia uchaguzi,” zilieleza taarifa hizo.
“Atazungumzia
kwa kina uchaguzi ulivyokuwa na kujibu maswali ya watu wa kada
mbalimbali waliokuwa wakihoji nini hatima ya CUF, baada ya kususia
uchaguzi na hivyo kupoteza nafasi za uwakilishi.”
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment