Mfumuko wa Bei kwa Machi 2016 umepungua hadi asilimia 5.4 kutoka asilimia 5.6 ya Februari.
Akizungumza
na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu
na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kuwa upandaji wa bei za
bidhaa kwa mwaka ulioshia kwa Machi , 2016 imepungua ikilinganishwa na
kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioshia Februari mwaka huu.
Amesema Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 101.93 mwenzi Machi, 2016 kutoka 96.69 mwezi Machi 2015.
Kwesigabo
amesema kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa
mwezi Machi, 2016 umepungua hadi asilimia 8.5 kutoka 9.5 iliyokuwa kwa
Februari, 2016.
Amesema
kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Machi, 2016 kumechangiwa hasa na
kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia
mwezi Machi 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Machi 2015.
Kwesigabo
amesema mwenendo wa bei za bidhaa zisizo za vyakula zinaonyeshwa
kupungua kwa mwezi Machi 2016 ikilinganishwa na mwezi Machi 2015 bidhaa
hizo ni Gesi asilimia 10, Diseli 5.8, Mafuta 1.0.
Mfumko
wa bei unafanana nchi za Afrika Mashariki , kwa mwezi Machi nchi ya
Kenya Mfumuko umepungua hadi asilimia 6.45 kutoka asilimia 6.8 kwa
Februari, Uganda mfumuko wa bei umepungua hadi asilimia 6.2 kwa Machi
2016 kutoka asilimia 7.0 kwa Februari 2016.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment