Serikali
ya Marekani imeihakikishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kuendeleza uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na
kutoa ufadhili na misaada mbalimbali ya miradi ya maendeleo hasa katika
sekta za afya na Elimu.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari muda mfupi mara baada
ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini aliyeongozana na
Ujumbe wa watu 15 wanaoshughulikia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na
Serikali ya Marekani hapa nchini, Waziri wa Mambo ya Nje,Afrika
Mashariki,Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa Dr Augustine Mahiga
alisema kuwa licha ya kutokea kutoelewana kwa Serikali hiyo na Tanzania
hivi karibuni lakini nchi hiyo imesema kuwa haitasitisha kuendeleza
miradi muhimu kama vile miradi ya Elimu na Afya iliyoanzishwa hapa
nchini na Seikali ya Marekani sambasamba na kuendeleza Ushirikiano huo
katika nyanja zingine za kimaendeleo.
Aidha
Waziri Dr Mahiga aliwatoa hofu watanzania na kusema kuwa miradi yote
ambayo ilianzishwa hapa nchini kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani
itaendelezwa kama ilivyopangwa hapo awali na kuahidi miradi mingine
zaidi itakayoleta tija kwa Taifa sambamba na kuleta ajira kwa Watanzania
walio wengi.
Kwa
Upande wake Balozi wa Tanzania Nchini Mark Childress alisema kuwa upo
umuhimu wa kuendeleza mahusiano kati ya Tanzania na Marekani hasa katika
utoaji wa misaada mbalimbali ya kimaendeleo hivyo Serikali ya nchi hiyo
itaendeleza na kukuza mahusiano hayo licha ya changamoto mbalimbali za
kisiasa zilipo nchini.
Nchi
hiyo ya Marekani imeahidi kuongeza miradi mingi zaidi nchini
itakayolenga kukuza uchumi wa Tanzania na kuitoa nchi hiyo katika hali
ya umasikini iliyopo hivi sasa.
Katika
mazungumzo hayo, pia walijadili jinsi ya kuimarisha masuala ya
kidiplomasia na namna ya kuzidisa usalama wa kikanda kwa manufaa ya
wote.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment