Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga inatarajia kuwafikisha mahakamani watumishi hewa 14
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Adrian Jungu aliwaambia waandishi wa
habari ofisini kwake juzi kuhusiana na hatua iliyochukua baada ya
kubainika kuwa halmashauri yake ina watumishi hao hewa.
Jungu
alisema mwanasheria wa halmashauri hiyo anaandaa utaratibu wa
kuwafikisha mahakamani watumishi hao ambao walikuwa wakipokea mishahara
wakati hawapo katika vituo vyao vya kazi.
Alisema watumishi hao ni walimu na hakukuwa na taarifa zozote za sababu za kutokuwapo kwao katika vituo vyao vya kazi.
“Nitawachukulia
pia hatua kali wakuu wa idara ambao watabainika walikuwa na watumishi
ambao hawakuwa katika vituo vyao vya kazi bila taarifa,” alisema.
Alisema adhabu hiyo itawakumba pia walimu wakuu wa shule kwa kosa la kushindwa kuripoti utoro wa walimu hao kwenye idara husika.
Mkurugenzi huyo aliahidi kuendeleza kazi ya uhakiki watumishi kila baada ya miezi sita ili kukomesha tabia hiyo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment