Kauli ya C.E.O wa Azam FC Baada ya Timu Yake Kunyang’anywa Point Tatu na Magoli Matatu

Jana May 5 2016 shirikisho la soka Tanzania TFF limetangaza rasmi kuwa klabu ya Azam FC imenyang’anywa point tatu na magoli matatu kutokana na kumtumia Erasto Nyoni ambaye alikuwa na kadi tatu za njano, katika mchezo wa 156 wa Ligi Kuu uliokuwa unazihusisha timu za Azam FC dhidi ya Mbeya City.

Baada ya taarifa hizo kutoka Sports Extra ya Clouds FM ilizungumza na afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Azam FC Saad Kawemba na kueleza “Kwa sasa tumewapatia hilo suala benchi la ufundi ili waweze kufuatilia na kuona uhalisia wa hicho kinachozungumzwa halafu watatueleza kama ni kweli kosa hilo limefanyika halafu tutajua nini cha kufanya” 

Maamuzi ya TFF kuinyang’anya point tatu na magoli matatu  Azam FC yanatokana na Kanuni ya 37(4) ya Ligi Kuu Toleo la 2015 inayoelekeza kuwa mchezaji atakayeonywa kwa kadi ya njano katika michezo mitatu hataruhusiwa kucheza mchezo unaofuata wa timu yake.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment