Zaidi ya wafanyabiashara wadogo 2,000 waliokuwa wakifanya shughuli zao
maeneo yasiyo rasmi katika Manispaa ya Ilala, wametengewa masoko manne
kwa ajili ya kufanya biashara.
Masoko hayo ni Kigogo Fresh
lililopo eneo la Pugu, Ukonga karibu na gereza, Tabata Muslim na Kivule
ambayo wafanyabiashara hao maarufu kama wamachinga wanatakiwa kwenda.
Wafanyabiashara
waliolengwa zaidi ni wale ambao wanafanya shughuli zao kwa kupanga
barabarani, hususan barabara ya mabasi yaendayo haraka na katika mitaa
mbalimbali ya Kariakoo na Mnazi Mmoja kwenye manispaa hiyo.
Baadhi ya
wafanyabishara hao walionyesha wasiwasi wao juu ya uamuzi huo kuwa
masoko hayo siyo rafiki kwao kwa biashara wanazozifanya.
Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi alisema jana kuwa, utaratibu wa
kuwapangia maeneo wafanyabiashara hao ulichelewa kwa sababu walikuwa
katika mchakato wa kuwatambua ili mpango wa kuwapeleka ufanyike kwa
ufanisi.
Alisema mazingira ya masoko hayo manne yapo vizuri na
yana uwezo wa kumudu wafanyabiashara zaidi ya 2,000 na makadirio ni
wafanyabiashara 6,000.
Kwa mujibu wa Mngulumi, kesho, manispaa
ikishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama itaanza operesheni ya
kuwaondoa kwa nguvu.
“Hapa ni kama nakazia tu uamuzi huu, ila
tulishawatangazia awali. Kwa hiyo sitarajii kuona watu maeneo hayo
kesho, operesheni hii itaenda sambamba na kuwaondoa wenye gereji bubu na
wanaoosha magari,” alisisitiza.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment