Mbunge
wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) ametolewa nje ya Bunge baada ya
kutaka kumkwida Mbunge wa Kasulu Vijijini, Agustine Holle (CCM) aliyedai
kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Kibamba,
John Mnyika wote wa Chadema kuwa wanaugua kichaa.
Waitara
alionesha kukerwa na kauli hiyo hasa pale Holle alipokataa kufuta kauli
yake, licha ya kutakiwa kufanya hivyo na Naibu Spika, Dk Tulia Akson.
Wakati
Holle akichangia, Waitara alinyanyuka kwenye kiti chake na alipofika
alipo mbunge huyo alimzungumzisha maneno ambayo hayakusikika na kuonesha
kama kutaka kumpiga kabla ya kukaa kwenye kiti kilicho mbele yake
ndipo, Holle alisikika akisema “wewe unataka nini” ndipo Naibu Spika
alipogundua kuwa Waitara anataka kumpiga Holle na kumuamuru atoke nje
lakini hakutii amri hiyo.
Kutokana
na kutotii, Naibu Spika aliamuru askari wamtoe ndipo walipoingia zaidi
ya askari watano na kutoka naye hadi nje ya geti kubwa la kuingilia
bungeni.
Holle
wakati anachangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa
fedha 2016/2017, alimtaja Lissu ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara hiyo
kuwa ana taarifa kuwa Lissu amewahi kuugua ugonjwa wa kichaa na hadi
sasa ana faili kwenye Hospitali ya Vichaa ya Mirembe iliyopo mkoani
Dodoma.
Hata hivyo, alipopewa nafasi na Naibu Spika kufuta kauli yake akasema “nafuta
kauli yangu lakini kwa taarifa zilizozagaa nimeamini ni kweli na mbona
kwao(Chadema) wapo wengi hata Mnyika sasa hivi yupo Muhimbili anatibiwa
kichaa”.
Kutokana
na kauli hiyo, Lissu alisema licha ya kuifahamu Hospitali ya Mirembe,
hajawahi hata kuingia kwenye geti la hospitali hiyo wala kuugua ugonjwa
huo na kutaka kiti cha Naibu Spika kimtake Holle athibitishe ; na
akishindwa kanuni zielekeze hatua za kuchukua kama zilivyowekwa.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment