DONALD TRUMP Amkubali SADAM HUSSEIN

MGOMBEA urais wa Chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amemsifu kiongozi wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein akisema aliweza kukabiliana vyema na magaidi.Bw Trump alikuwa akihutubia mkutano wa kampeni eneo jimbo la North Carolina Jumanne alioanza kuzungumza kuhusu kiongozi huyo aliyeuawa kwa kunyongwa Desemba 2006.“Saddam Hussein alikuwa mbaya, kweli? … Lakini mnafahamu ni jambo gani aliweza kulifanya vyema sana? Aliwaua magaidi. Alifanya hivyo vyema sana,” Trump alisema.

“Hawakuwasomea haki zao, hawakunena lolote. Walikuwa magaidi, mambo yao kwisha.”Bw Trump awali amewahi kusema kwamba ulimwengu ungelikuwa “asilimia 100 bora kuliko sasa” iwapo viongozi wa kiimla kama Saddam Hussein na kiongozi wa muda mrefu wa Libya, Muammar Gaddafi wangelikuwa bado uongozini.

Kabla ya uvamizi ulioongozwa na Marekani, ambapo Saddam aliondolewa madarakani, Iraq ilikuwa imeorodheshwa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani kama taifa linalofadhili ugaidi.
Afisa mkuu mshauri wa Hillary Clinton kuhusu sera, amejibu matamshi ya Bw Trump kwa kusema kuwa: “Sifa za Donald Trump kwa viongozi wa kiimla yamkini hazina mipaka.”
Amesema matamshi kama hayo yanaashiria “ni jinsi gani itakuwa hatari (kuwa na Trump) kuwa Amiri Jeshi Mkuu na jinsi ambavyo hafai kuhudumu kama rais.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment