Balotelli: Najutia Sana Kujiunga na Liverpool

“Kujiunga na Liverpool, huu ulikuwa uamuzi mbaya zaidi aliowahi kuufanya maishani mwake”, Adai Balotelli
Mwitaliano huyo alifunga mabao manne katika mechi 28 alizochezea Liverpool baada ya kujiunga nao kutoka AC Milan mwaka 2014 kwa thamani ya dola milioni 16.
“Isipokuwa mashabiki, ambao hunishabikia, na wachezaji kadhaa ambao tunasikilizana, sipendi klabu yenyewe,” Balotelli ameiambia runinga ya Ufaransa ya Canal Plus.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alisema hayo kabla ya kufunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza na klabu ya Nice katika michuano ya Ligue 1 walipofunga mabao 3-2 dhidi ya Marseille siku ya Jumapili.

Meneja Brendan Rodgers, aliyemsajili Balotelli, alipigwa kalamu na Liverpool mwezi Oktoba mwaka 2015, na Jurgen Klopp akachukua hatamu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment