Mwenyekiti
wa Taasisi inayoshughulikia masuala ya Afrika (Africa Matters Limited)
Mhe. (Baroness) Lynda Chalker wa Wallasey - Uingereza, amempongeza Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi
kubwa alizozifanya kupiga vita rushwa na kujenga mazingira bora zaidi
kwa uwekezaji.
Mhe.
Lynda Chalker ametoa pongezi hizo jana tarehe 31 Agosti, 2016 Ikulu
Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli
kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo hali ya uwekezaji hapa nchini.
"Mhe
Rais amefanya uamuzi sahihi wa kupiga vita rushwa na kuiweka nchi hii
katika njia mpya ya uwekezaji mzuri na hicho ndicho tumekuwa
tukikizungumza, nimejitahidi kutoa ushauri wangu wa namna mimi na
kampuni yangu binafsi tunaweza kumsaidia, nionavyo mambo yanakwenda
katika mwelekeo mzuri" Amesema Mhe. Lynda Chalker.
Kwa
Upande wake Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Lynda Chalker kwa ushauri na
dhamira yake ya kutaka Tanzania ipige hatua kimaendeleo na amemuomba
kutumia ushawishi wake kuwahamasisha wawekezaji mbalimbali kutoka nchini
Uingereza na kwingineko duniani kuja kuwekeza nchini Tanzania ili
kuharakisha zaidi maendeleo.
Hata hivyo Dkt. Magufuli amesema wawekezaji wanaokuja Tanzania hawana budi kuwa wawekezaji makini.
"Ninawakaribisha
wawekezaji makini kutoka Uingereza na mahali popote dunia, lakini
nisingependa kupata wawekezaji wababaishaji" Amesisitiza Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
31 Agosti, 2016
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment