KAFULILA Kukata Rufaa Kupinga Uamuzi wa Mahakama!

Aliyekua Mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, kupitia chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila amesema ataka rufaa kupinga kushindwa kesi ya uchaguzi dhidi ya Mbunge alieshinda jimbo hilo kupitia chama cha Mapinduzi(CCM), Bi. Hasna Mwilima.

Aliekua Mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, kupitia chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila.
Akiongea mara baada ya kutolewa hukumu ya kesi yake ya kupinga ushindi wa Bi. Hasna Mwilima amesema kuwa Mahakama Kuu imeshindwa kuwasilisha fomu muhimu ambazo ni vilelezo tosha vya ushindi wake katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 Mwaka Jana.

Kwa upande wake Mbunge mteule wa jimbo hilo Bi. Hasna Mwilima amemtaka Mbunge huyo wa Zamani wa jimbo hilo kushirikiana nae katika kuliletea maendeleo jimbo hilo kwa kuwa yeye alishindwa kufanya hivyo pale alipopewa dhamana ya kufanya hivyo.

Moja kati ya Mambo yaliyotajwa na Jaji wa Mahakama Kuu Ferndand Wamari, kunyima ushindi Kafulila ni kushindwa kuwasilisha nakala zote za matokeo ya fomu namba 21 B, ya pande zote mbili ili kuthibitisha uhalali wa anachodai ni batili,

Pia kutokuwa na ufanano kati ya Takwimu za Kafulila na zile za wakala wake Elias Kitui, Hivyo kutia shaka ambapo mahakama ikawa imesalia kuamini matokeo ya tume.

Kwa mujibu wa Jaji katika maombi matatu ya msingi, David Kafulila, alitaka Mahakama ibatilishe matokeo ishinikize tume kumtangaza mshindi au itoe unafuu kwa walalamikiwa jambo ambalo amesema kati ya yote hakuna ushahidi ambao utaifanya mahakama kuamua hivyo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment