Mayanja: TFF Imeipa YANGA SC Ubingwa


jackson-mayanja_16c1zw8tqege81g3qbstgngm9zKocha wa Simba, Jackson Mayanja.
Omary Mdose na Nicodemus Jonas
BAADA ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kurekebisha ratiba ya Ligi Kuu Bara, Kocha wa Simba, Jackson Mayanja ameibuka na kusema ratiba hiyo kwa sasa itazibeba timu za Yanga na Azam.

TFF ilirekebisha ratiba na kuitoa katikati ya wiki iliyopita ambapo ndani yake imeorodhesha siku na tarehe ambazo mechi za viporo za Yanga na Azam zitachezwa ili kuwa sawa kimichezo na timu nyingine ikiwemo Simba.

Awali, kabla ya kutoka kwa ratiba hiyo, viongozi wa Simba walipeleka barua TFF kuitaka ifanye haraka iwezekanavyo kuhakikisha viporo vya Yanga na Azam vinachezwa huku wakitishia kutoipeleka timu uwanjani kama hilo halitafanyiwa kazi.

Ratiba ya sasa itawafanya Yanga na Azam kucheza si chini ya mechi tatu ndani ya siku 11, kitendo ambacho Mayanja anaona kina faida kubwa kwa wachezaji kujiweka fiti na kinaweza kuwasaidia kutwaa ubingwa.

“Ratiba hii ya sasa ni nzuri kwa Yanga na Azam na timu hizo zinaweza kufanya vizuri kwenye ligi pamoja na michuano ya kimataifa, kokote pale wachezaji wanatakiwa kucheza mara kwa mara na siyo kukaa muda mrefu wakiwa wamepumzika.

“Nashangaa kusikia wanailalamikia, hawajui kama itawawezesha kutambua upungufu wa wachezaji wao ikiwemo katika suala zima la pumzi na ufiti, wanachotakiwa ni kuishukuru TFF kwa kuwasaidia kwa hilo ambalo litawaweka sehemu nzuri kwenye mbio za ubingwa,” alisema Mayanja.

Huku Mayanja akisema hayo, hivi karibuni Ofisa Habari wa Azam, Jafar Idd, alinukuliwa akisema wanajipanga kupeleka barua TFF kuliomba shirikisho hilo liifanyie tena marekebisho ratiba hiyo mpya kwani itawachosha wachezaji wao kwa jinsi ilivyo.
Simba kwa sasa ipo kileleni ikiwa na pointi 57, ikiwa imecheza michezo 24 ikifuatiwa na Yanga wenye pointi 50 lakini wakiwa wamecheza michezo 21.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment