Wachezaji Ahly Kuchomwa Sindano Waivae YANGA SC

2014-635463852849612098-961Wachezaji wa Al Ahly.
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
UNAWEZA kusema kweli Al Ahly wameamua kujiandaa kweli kabla ya kuwavaa Yanga katika mechi ya Jumamosi ya Aprili 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kabla ya mechi hiyo ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya 16 Bora, wachezaji wa Al Ahly watachomwa sindano maalum ambazo zinaelezwa kuwa ni za kinga.
Sindano hizo zinaelezwa ni kwa ajili ya kinga ya malaria, ugonjwa ambao ni adimu nchini Misri.

“Kweli utaratibu huo unafanywa ili wachomwe sindano. Haijajulikana lakini huenda ikawa wiki ijayo baada ya Ahly kuwa wamecheza mechi yao ya Kombe la Egypt dhidi ya timu ya daraja la kwanza itakayochezwa Alhamisi,” kilieleza chanzo cha uhakika kutoka Cairo.

“Ahly wamezoea kufanya hivyo, wanachoma sindano hizo kila wanapokaribia kwenda kucheza katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.”
Al Ahly inatarajia kuwasili nchini Aprili 5 ambayo itakuwa ni Jumanne, tayari kwa ajili ya mechi hiyo Jumamosi inayofuata.

Hadi sasa, Ahly inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Misri ikiwa na pointi 67 na Zamalek ambao ni wapinzani wao wakubwa wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 61.
Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ngumu kwa timu zote mbili huku ile ya pili ugenini ikipewa nafasi ya kuamua matokeo ya mchezo.
Miaka mitatu iliyopita timu hizo zilikutana na Ahly kufanikiwa kuitoa Yanga kwa mikwaju ya penalti ikiwa ni baada ya Waarabu hao kufungwa bao 1-0 jijini Dar na wenyewe wakalipa kipigo kama hicho jijini Alexandria.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment