Wizara mbalimbali za Serikali hii ya awamu ya tano zinazidi kuingia kwenye headline, ikiwa ni siku kadhaa zimepita baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga
kuagiza idara ya uhamiaji ifanyiwe mabadiliko makubwa ili kuboresha
huduma na kuimarisha uadilifu katika vitengo vya idara hiyo nyeti.
Leo March 18 2016 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Idara ya Uhamiaji imefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa maofisa 14 waandamizi katika Ofisi ya Makao Makuu, Mikoa, Wilaya na Vituo vya mipakani.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari
Kaimu Kamishna wa Utawala na Fedha Idara ya Uhamiaji, Abass Mussa
Irovya ameleza kuwa hatua hiyo ya kubadilishia vituo ni endelevu na ni
kwa maofisa zaidi ya mia mbili. Irovya amesema ‘Idara
ya uhamiaji inaendelea na utaratibu wa kuwabadilisha vituo vya kazi
Maofisa zaidi ya mia mbili kutoka sehemu mbalimbali nchini ikiwa ni
Agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga‘
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment