AZAM FC Yaamua Liwalo na Liwe

Omary Mdose, Dar es Salaam
SIKU sita kabla Azam FC haijavaana na Esperance Sportive de Tunis ya Tunisia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho, timu hiyo itakuwa ugenini kucheza na Toto Africans ya Mwanza mechi ya Ligi Kuu Bara.
Kocha wa Azam, Stewart Hall ameamua ‘kujilipua’ kwa kutumia silaha zake zote katika mchezo huo akiweka pembeni hofu ya kuumia kuelekea mechi dhidi ya Esperance.

Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba aliliambia Championi Jumamosi kwamba, mechi ya Toto itakayochezwa badae leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ni muhimu kwao katika harakati za kutwaa ubingwa wa ligi kuu.
Azam ipo nafasi ya tatu katika ligi kuu ikiwa na pointi 50 sawa na Yanga iliyo nafasi ya pili huku Simba ikiongoza na pointi 57. Azam na Yanga zina mechi 21 huku Simba ikicheza 24.

Kawemba alisema: “Tuna mechi ngumu mfululizo na zote ni muhimu kwetu, siku chache kabla ya kucheza na Esperance tutakuwa na mchezo wa ligi ugenini dhidi ya Toto, tunataka ushindi katika mechi zote.
“Hakuna haja ya kuwapumzisha wachezaji kwa ajili ya mchezo unaofuata na badala yake tutachezesha mziki kamili, tumeamua hilo jambo kwani ni la manufaa kwa timu.”
Ikimaliza mechi na Toto, Jumatano ijayo itacheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam halafu itacheza na Esperance, Aprili 10, mwaka huu uwanjani hapo.

-GPL
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment