Mchezaji wa Yanga, Donald Ngomaakifanya yake na kocha wake, Hans van Der Pluijm.
Khadija Mngwai,Dar es Salaam
STRAIKA wa Yanga, Donald Ngoma amewaambia mashabiki na
wachezaji wenzake kwamba hakuna haja ya kuogopa kucheza mechi nne ndani
ya siku kumi kwani wanapaswa kujituma tu ili ushindi upatikane.
Tayari Yanga imeshacheza dhidi ya Ndanda FC, juzi katika Kombe la FA,
lakini leo inacheza na Kagera Sugar mchezo wa Ligi Kuu Bara na
Jumatano ijayo inapambana na Mtibwa Sugar halafu Jumamosi ndipo icheze
na Al Ahly ya Misri mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia.
Yanga yenyewe ilishalalamikia ratiba hiyo ikiamini inainyima muda wa
kujiandaa zaidi na mechi dhidi ya Al Ahly ya Misri ambayo inaonekana
kuwa ngumu kwao.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Ngoma raia wa
Zimbabwe alisema siyo jambo la kawaida kwa timu kucheza mechi nne ndani
ya siku 10, lakini hawapaswi kulalamika au kuogopa badala yake
wanatakiwa kupambana kuhakikisha wanashinda mechi zote.
“Kuhusu kucheza mechi mfululizo siyo jambo la kawaida kwa timu
kucheza mechi nne ndani ya siku 10, tunachotakiwa ni kuhakikisha
tunafanya vizuri na kushinda.
“Hatuhitaji kulalamika kama wachezaji na tunachotakiwa ni kujituma na
kupambana kwa kuonyesha uwezo katika kila mchezo, kwani uwezo huo
tunao,” alisema Ngoma.
-Championi
-Championi
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment