Steve NYERERE Amtwisha Jukumu la Filamu Paul MAKONDA


stevevee.jpgSteve Nyerere
Stori: MAYASA MARIWATA
MSANII wa filamu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameshikilia bango la kutaka filamu za nje zizuiwe hapa nchini kwa kuamini kuwa, soko la filamu za Kibongo litazidi kutanuka na kufanya vizuri.
Paul-Makonda (1)Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, kila anapofikiria masuala ya filamu jambo hilo huwa linazidi kumnyima raha na kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kulishughulikia kwa kuwa yeye ni kiongozi wa serikali kuhakikisha wasanii wa filamu za Kibongo wanakuwa na amani katika kazi zao.
“Nimefurahi sana Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar. Namuomba alifanyie kazi suala la filamu za kigeni, ahakikishe hazipati nafasi kubwa isipokuwa filamu zetu,” alisema Steve.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment