Bibi wa mtoto huyo.
NA GLADNESS MALLYA
Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Huu ni ukatili wa
kutisha! Mtoto mwenye umri wa miaka tisa (jina linahifadhiwa) mkazi wa
Mji Mpya, Kata ya Saranga jijini Dar, amedaiwa kufanyiwa ukatili wa
kuvutishwa bangi, kunyweshwa madawa ya kulevya kisha kulawitiwa na
kijana aliyetambulika kwa jina la Ibrahimu.
Akizungumza kwa huzuni, mtoto huyo
alisema kijana huyo humuita akiwa anacheza na kumpeleka chumbani kwake
ambako humlewesha kwanza ili kumpoteza fahamu, lakini anapozinduka
hujikuta amelawitiwa.
Eneo anakoishi mtuhumiwa.
“Ibrahimu alikuwa akinivutisha bangi,
anachukua maji anachanganya na unga ananinywesha kwa lazima,
akishamaliza hivyo nakuwa sijielewi ndipo anaponilalia na kunifanyia
vitendo hivyo.
“Alikuwa akinipa hela, siku ya kwanza
alinipa 2,400 akaniambia nisiseme, nikisema ataniua, hivyo nikawa
nanyamaza, sikuwaambia bibi wala babu, siku nyingine alinituma nije
nichome nyumba ili wafe, anichukue nikakae naye kwake, nikaja nikawasha
moto lakini walishtuka na kuja kuuzima,” alisema mtoto huyo.
Babu wa mtoto huyo aitwaye Daudi,
alisema aligundua kwamba mjukuu wake hayupo sawa kutokana na kushindwa
kutembea vizuri pamoja na kushindwa kukaa ndipo alipoamua kumkagua na
kukuta ameharibika vibaya sehemu za siri.
Mtoto anayedaiwa kuvutishwa bangi na kulatiwa.
Baada ya kushuhudia tukio hilo,
alikwenda kutoa taarifa kwa mjumbe wa nyumba kumi aliyemtaja kwa jina
moja la Said, Novemba mwaka jana, lakini hakuna hatua zozote alizochukua
zaidi ya kuwaambia anafanya uchunguzi.
“Kiukweli mjukuu wangu alikuwa anatembea
kwa shida, nguo alizovaa zilichafuka sana na akienda chooni alitoa
damu, kitu kilichombadili tabia, akaanza kuwa mkorofi huku akisinzia
kama teja.
“Ilibidi bibi yake arudi tena kwa mjumbe
wa nyumba kumi ambaye alimpa barua na kupeleka ya serikali za mtaa,
maana sisi tulishindwa kwenda polisi.
“Tuangalie sisi tumeshakuwa watu wazima,
tumeshindwa tufanyeje, tunaomba msaada kwa Watanzania wenzetu
watusaidie ili huyu kijana akamatwe maana anamtuma huyu mtoto aje
atuchomee moto huku ndani, tunaishi kwa wasiwasi sana,” alisema babu
huyo.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Christopher Fuime
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Mji Mpya,
Daniel Mumba alithibitisha kupokea barua ya mjumbe ambapo alimhoji mtoto
na kumweleza vitendo hivyo vya kikatili anavyofanyiwa na kuchukua
jukumu la kwenda nao katika Kituo cha Polisi Kimara Temboni na kufungua
kesi yenye namba KMR/RB/4480/2016 KULAWITI.
Aidha, mwenyekiti huyo alilaani vikali
kitendo cha mjumbe huyo kutolifanyia kazi suala hilo mapema na kuchukua
muda mrefu jambo ambalo siyo sahihi, hivyo kuwataka wajumbe wa mitaa
kutimiza majukumu yao na kuepuka kuwalinda wahalifu.
Alipotafutwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi
wa Kinondoni, ACP Christopher Fuime kuhusiana na tukio hilo, simu yake
iliita bila kupokelewa hadi tunakwenda mitamboni.
-GPL
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment