Hatimaye SIMBA SC Waamua Kuchukua Maamuzi Mazito Baada ya Mashabiki Wao Kucharuka

Baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba April 20 2016 kupitia kwa kocha mkuu Jackson Mayanja, afisa habari wake Haji Manara, nahodha wa timu Musa Mgosi pamoja na meneja wa timu Abasi wamejitokeza na kuongea na waandishi wa habari.

Viongozi hao wa Simba wamejitokeza na kuomba radhi mashabiki wa Simba ambao awali baada ya mchezo dhidi ya Toto Africans kumalizika kwa kufungwa goli 1-0 walimfuata Makamu wa Rais wa Simba Geofrey Kaburu na mwenyekiti wa kamati ya Usajili Zacharia Hans poppe na kuwatolea maneno yasio ya kiungwana pamoja na kutishia kuchoma basi la Simba.

Pamoja na hayo Simba kupitia kwa afisa habari wake Haji Manara wametangaza kumuongezea adhabu beki wake wa kulia Hassan Kessy kutokana na kuoneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumchezea faulo mbaya Edward Christopher, kitendo ambacho kilimfanya muamuzi wa mechi amuoneshe kadi nyekundu ya moja kwa moja.

“Kessy juzi ameigharimu timu hatujui kwa makusudi au bahati mbaya, Kessy ameigharimu timu kwa kucheza rafu mbaya tena yenye nia mbaya kwa Edward Christopher kwa kumpandishia mguu kichwani kwa makusudi, licha ya kuoneshwa kadi nyekundu na refa na kukosa mechi mbili, Simba inamuongezea adhabu na kumfungia mechi 5” >>> Haji Manara
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment