INAUMA SANA: Undani Familia Iliyofukiwa na Udongo Kawe Jijini Dar


IMG_1988Majeneza matatu ya familia moja yakiwa tayari kwa ajili ya kuagwa.
IMG_1983 
Marehemu Efrem Manguli ambaye ni baba wa watoto wawili  Fredy Manguli na Daniel Manguli ambao nao walifariki.
Stori: Makongoro Oging’ na Issa Mnally, UWAZI DAR ES SALAAM: Maporomoko ya karo la maji machafu yaliyotoka kwenye nyumba ya jirani na kutua kwenye nyumba nyingine kisha kuua watu watano na wengine kujeruhiwa, bado simulizi yake inauma sana, Uwazi limefuatilia kwa kina.
Tukio hilo ambalo bado ni gumzo kila kona ya nchi hususan jijini Dar es Salaam, lilijiri alfajiri ya Aprili 6, mwaka huu katika Kitongoji cha Kawe –Ukwamani wilayani Kinondoni, Dar.
Waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Efrem Manguli (47), Daniel Manguli (5), Fredy Manguli (2), Maria Iyesi (12) na Grayson Clarence (3) ambaye mwili wake ulizikwa Mbezi Beach, Alhamisi iliyopita.
Grayson yeye ni mjukuu wa mwenye nyumba ambapo Manguli na familia yake walikuwa ni wapangaji.

IMG_1981Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Daniel Manguli likiandaliwa kwa ajili ya kuagwa.
FAMILIA AMEBAKI MKE TU
Katika tukio hilo, familia ya Manguli ilipotea yote, yaani baba na watoto wake wanne huku mke, mama Dani akibaki salama kwa vile wakati wa tukio hilo alikwenda kuuza chai na chapati maeneo ya Mbezi Beach, Dar na hicho ndicho kilichomuokoa.

Baada ya tukio hilo, mke huyo akiwa anarudi, alipigiwa simu na kupewa taarifa hizo ambapo hakuamini lakini alipokaribia nyumbani hapo na kuona umati wa watu, alianguka na kupoteza fahamu. Alichukuliwa na kupelekwa kwa ndugu yake, Mbezi Beach, baadaye akapelekwa kwenye msiba, Kinondoni Shamba.
IMG_1980Jeneza la marehemu Fredy Manguli.
KAWAIDA YA UWAZI
Kama ilivyo kawaida ya gazeti hili kila linapotokea tukio kubwa kufuatilia kwa undani, timu yetu ilifika eneo la tukio na kukuta wakazi wa eneo hilo wakiwa katika hali ya huzuni huku Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Assemblies of God ‘Mlima wa Moto’, Gertrude Rwakatare ambaye naye alikuwepo, akishindwa kujizuia na kutokwa machozi mara kwa mara.

Kwa mujibu wa majirani, wakati udongo huo unaporomoka, baadhi ya watu walikuwa bado wamelala majumbani mwao.
“Mimi nilikuwa bado kitandani kwa sababu ya hali ya hewa ya nje. Lakini nilikuwa macho. Mara nikasikia kishindo kizito tiii! Nikashtuka, sikujua ni nini! Mara tena nikasikia kelele za watu kama wanaomba msaada.
IMG_1988Majeneza matatu ya familia moja yakiwa tayari kwa ajili ya kuagwa.
“Nilitoka, nikakuta na majirani wengine wanatoka. Nikawauliza ni nini jamani? Mmoja akanyooshea mkono kwenye nyumba ya baba Dani (Efrem). Kufika tukashangaa kuona nyumba imeanguka chini na kelele zikitokea ndani.
“Miti iliyoporomoka na udongo ikafikia juu. Kama unaangalia hivi unaweza kusema imeotea hapo tangu zamani. Tulijaribu kumuita baba Dani huku tukifukua udongo lakini hakuitika. Tukajua ameshafariki dunia.
“Kusema kweli kama kuna vifo vibaya hapa duniani, baba Dani na watoto wake wamekufa vifo vibaya sana. Mungu amlaze mahali pema peponi yeye na familia yake,” alisema jirani mmoja ambaye hakupenda kujitambulisha jina lake.
IMG_2006Mfiwa akilia kwa simanzi kubwa.
Philip Thomas Manguli ni baba mzazi wa marehemu Efrem. Katika mahojiano na gazeti hili,  Kinondoni Shamba palipowekwa msiba, alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi nilikuwa kazini, asubuhi nikawa natoka narudi hapa kwangu. Nilipofika maeneo ya Biafra nikapigiwa simu na shemeji yangu na kuniambia kuna taarifa mbaya ya mwanangu Efrem na watoto wake wamefariki dunia kwa kuangukiwa na kifusi cha udongo. Nilidondoka chini sikuwa na nguvu ya kutembea. Nikachukuliwa na watu wanaonifahamu kunileta hapa nyumbani.”

TAARIFA ZAMKUTA MAMA MZAZI AKIOSHA VYOMBO
“Nilimkuta mke wangu nje akiosha vyombo, nikamwambia familia yetu imekwisha. Efrem  na watoto wake wote akina Fredy wamefariki dunia (akaanza kulia).

IMG_1996“Kilio kilianza hapo. Tukalia wote na nyumba nzima baada ya kuelezwa kukalipuka vilio. Baadaye huyo shemeji yangu aliyenipigia simu, alikuja nyumbani na kutueleza vizuri kuhusu vifo hivyo.” 

SIKU MBILI NYUMA, EFREM ALIPELEKA MSIBA MORO
“Kinachoniuma zaidi, marehemu Efrem amepatwa na mauti siku mbili tu tangu tumerudi kutoka Morogoro ambako tulipeleka msiba wa mdogo wangu. Yaani yeye anamwita baba mdogo marehemu tuliyempeleka.” 

BABA HATASAHAU
“Mimi sitasahau tukio hili katika maisha yangu. Nimepata pigo kubwa mno, familia yangu imetetereka, imepotea,” akaanza kulia.
IMG_2000MSIKIE NA HUYU
Akizungumza na gazeti hili huku machozi yakimchuruzika muda wote, Sando Hamisi ambaye ni wifi wa marehemu Maria, alisema:

“Mimi ndiye niliyemleta Maria hapa Dar kutoka Kijiji cha Nyabisaga wilayani Tarime, Mkoa wa Mara na kumuweka  kuishi na familia ya Manguli. Baada ya kifo chake, wazazi wake waliambiwa na wakasema wanakuja ili kumsindikiza mtoto wao makaburini.” 

WAKAZI WAANZA KUHAMA
Baadhi ya watu waliliambia Uwazi kuwa ujenzi wa eneo hilo ni hatarishi kwa makazi ya watu kwani kuna sehemu nyumba zinaonekana kwa chini nyingine kwa juu. Hivyo maporomoko ni jambo linalotarajiwa wakati wowote ule.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo wameanza kuhama kuhofia maisha yao na haikujulikana mara moja wanakohamia.

IMG_1990Waombolezaji wakiwa msibani.
MAZISHI MARA MBILI
Efrem na watoto wake walizikwa Jumamosi iliyopita kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar huku gazeti hili likibaini kwamba kwamba kulikuwa na makosa ya tarehe waliyofariki iliyoandikwa kwenye misalaba yao. Badala ya kuandikwa 06.04.2016, iliandikwa 06.03.2016.
Maria alizikwa Jumapili kwenye makaburi hayohayo. Kuchelewa kuzikwa kwa Maria kulitokana na kuchelewa kufika kwa wazazi wake.
Mungu aziweke pema peponi, roho za marehemu wote. Amina.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment