MKE
wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa amewaomba wananchi wa wilaya ya Ruangwa
kuwaombea dua viongozi wa taifa, Rais Dk. John Magufuli, Makamu wa Rais,
Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili waweze kufanya
kazi zao kikamilifu.
Amesema
kazi nzito inayofanywa na viongozi hao ya kuhakikisha nchi inakuwa
salama na inasonga mbele kimaendeleo ni shughuli ngumu na inahitaji
nguvu ya Mungu, hivyo ni vema wananchi wakawaombea dua ili kazi hiyo
iweze kuwa na tija kwao na taifa kwa ujumla.
Mke
wa Waziri Mkuu ameyasema hayo jana alipozungumza na wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Chinongwe wilayani
Ruangwa, ambapo amewaomba mwananchi hao wajitahidi kuwaombea dua
viongozi hao ili malengo yao ya kuwaletea maendeleo yatimie.
Mary
ameongozana na Waziri Mkuu Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa, katika
ziara yake ya kuwashukuru wananchi waliomchagua kwa nafasi ya ubunge na
kisha Rais Dk Magufuli kumteua kuwa kushika wadhifa huo.
"Nawashukuru
sana wananchi kwa kuwa kura zenu ndiyo zilizosababisha Mheshimiwa
Majaliwa ambaye ni mbunge wetu kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, hivyo
nawaahidi kuwa tutaendelea kushirikiana,” amesema mke wa Waziri Mkuu.
Amesema
licha ya kuongezewa majukumu atahakikisha anaendelea kushirikiana na
wanaruangwa ili waweze kuendeleza shughuli za maendeleo katika wilaya
hiyo na kwamba wasiwe na wasiwasi kwani hata wasahau kwa kuwa anawapenda
na kuwaheshimu.
Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment