Kamati
ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala imeipongeza Tume ya Taifa ya
Uchaguzi kwa kufanikisha kuendesha Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na
Madiwani wa mwaka 2015 vizuri na kuiacha nchi ikiwa na Amani, utulivu na
Usalama.
Hayo
yalisemwa jijini Dar ess Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati
hiyo Mh Najma Murtaza Giga walipokutana na Menejimenti ya Tume ya Taifa
ya Uchaguzi katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere convention Center katika
kikao mahsusi cha Kupitia Bajeti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka
wa fedha wa 2016/2017.
Aidha,
pongezi hizo kwa NEC zilitolewa na wajumbe wa pande zote mbili yaani wa
Chama tawala na wale wa upinzani wa kamati hiyo kwa nyakati tofauti.
Baadhi
ya wabunge hao ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mheshimiwa Najma
Murtaza Giga(CCM), Twahir Awesu Mohammed (CUF) na Nassor Suleiman Omar
(CUF).
Alisema
ni jambo la heri sana pale ambapo taasisi ama mtu anafanya kazi ya
kutukuka kupewa sifa yake na kupewa moyo ili aendelee na moyo wa
kufanya kazi kwa bidii na hatimaye kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi
si tu kwa manufaa ya taasisi yake bali hata kwa Taifa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhan aliiambia kamati
hiyo kwamba haikuwa kazi rahisi kuendesha na kusimamia Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2015 na Nchi ikaendelea kuwa na amani na utulivu kwani ushindani
wa kisiasa ulikuwa mkubwa kiasi cha kutishia maisha ya watanzania.
“Tulijitahidi
kwa kadiri ya uwezo wetu kufuata Sheria Kanuni na taratibu za kusimamia
Uchaguzi pamoja na kwamba Bajeti ilikua haitoshi hasa wakati tunaanza
zoezi la Uandikishaji wa Wapiga Kura kwa kutumia Teknolojia ya BVR
ambapo tulilazimika kuandikisha wapiga Kura kwa kuhamahama” Alisema Kailima.
Naye
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge Jenista
Mhagama aliwashukuru wabunge kwa niaba ya Serikali kwa jinsi
walivyothamini na kutambua Kazi kubwa iliyofanywa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi na kuahidi kufikisha Serikalini mawazo ya kuitafutia Tume fedha
kwaajili ya Tume kuzipatia Asasi za Kiraia zinazotoa Elimu ya Mpiga
Kura kwani lilijitokeza suala la Ukosefu wa Fedha za Kuendeshea Elimu
hiyo.
Bajeti
ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 ni jumla
ya Tsh 4,830,537.167/= ikiwa ni fedha za matumizi ya kawaida OC Miradi
ya Maendeleo pamoja na Mishahara ya watumishi.
Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2015 ulifanyika tarehe 25 Oktoba ambapo aliyekua Mgombea
Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh.Dkt John Pombe Magufuli
aliibuka Mshindi.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment