Ahmed Msangi , Kamanda wa Polisi Mkoani wa Mwanza akionyesha silaha aina
ya Ak 47 kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Ofisini kwake
Kamanda mpya wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed
Msangi amawataka polisi kukabiliana na majambazi kwa nguvu zote na
ikibidi kuwaua kabla hawajasababisha madhara makubwa kwa raia.
Msangi
ambaye amehamia mkoani Mwanza akitokea jijini Mbeya, ametoa kauli
hiyo leo wakati akizungumza na maofisa usalama na polisi wa vyeo
mbalimbali baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi hiyo na SACP, Justus
Kamugisha.
Msangi
ametoa kauli hio siku chache baada ya John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza kusema kwamba, Kamugisha alikuwa mzigo kwenye jiji hilo kutokana
na kushindwa kukabiliana na ujambazi.
Katika
kipindi cha miezi miwili ya Machi na Aprili mwaka huu, matukio saba ya
uhalifu wa kutumia silaha za moto yameripotiwa na katika matukio hayo
watu sita walipoteza maisha.
Msangi
amesema kuwa, anawashangaa polisi wanaoshindwa kutumia silaha zao
kuwakabili watu wanaodaiwa kuwa majambazi na kusababisha vitendo vya
uhalifu kuendelea kushamiri jijini humo.
“Tumieni
na nyie bunduki zenu kuyaua majambazi. Mbona wao wanaua raia?
Haiwezekana uwe na silaha halafu unaacha kuchukua hatua za haraka za
watu ambao wanasababisha mauaji na uporaji wa mali za raia,” amesema Msangi.
Msangi
amesema, Jiji la Mwanza miezi michache iliyopita limetikiswa na matukio
ya unyang’anyi wa kutumia silaha yanayoambatana na mauaji ya raia,
kujeruhi na uporaji wa mali zao.
Amesema kuwa, polisi wanapaswa kufanya kazi zao kwa kujiamini na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Kamanda
Kamugisha akikabidhi ofisi hiyo aliwahimiza polisi kufanya kazi kwa
weledi na kwa kuzingatia maadili ya jeshi hilo bila kumuonea mtu yeyote
yule.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment