NGOMA wa YANGA SC Abeba Rekodi Bab’Kubwa Misri

Wachezaji wa Yanga wakishangilia nastraika, Donald Ngoma (wa kwanza kushoto).
Abdallah Zalala, Pwani na Nicodemus Jonas
LICHA ya Yanga kufungwa mabao 2-1 na Al Ahly ya Misri kisha kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika juzi jijini Alexandria, straika, Donald Ngoma ameweka rekodi ya kipekee.
Straika huyo wa Yanga ambaye ni raia wa Zimbabwe, aliweka rekodi hiyo ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Yanga kufunga bao ndani ya dakika 90 tangu timu hizo zikutane zaidi ya mara nne nchini humo lakini pia kwa timu za Misri na Uarabuni, Yanga imekuwa ikipata tabu inapokuwa ugenini dhidi ya timu za ukanda huo.
Rekodi zinaonyesha kuwa mara ya mwisho kwa mchezaji wa Yanga kufunga bao ndani ya dakika 90 ilipocheza ugenini dhidi ya timu ya Misri na zile za ukanda huo kwa jumla ni mwaka 1992, ambapo Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ismailia jijini Cairo.
Pamoja na sare hiyo, bado Yanga iliondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa mwaka huo kwa kuwa katika mchezo wa awali Ismailia ilishinda mabao 2-0 jijini Dar. 

Katika mchezo wa juzi, Ngoma alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 57, lakini furaha yao hiyo ilikatishwa na bao la pili kwa Al Ahly lililofungwa katika dakika ya 95 ikiwa ni dakika ya mwisho katika zile za nyongeza.
Al Ahly na Yanga zimekutana mara nne nchini humo. Mara ya kwanza Yanga walifungwa 5-0, mara ya pili 4-0, ya tatu 1-0 na juzi walifungwa 2-1.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment