Picha 10: Dereva wa Kirikuu Anusurika Kifo Baada ya Gari Lake Kuwaka Moto

DSC_0439Gari lilivyokuwa kwa ndani baada ya kuwaka motoDSC_0440Askari wa Kikosi Maalum cha Zima Moto pamoja mashuhuda wa tukio hilo.DSC_0442Gari lilivyowaka.DSC_0446MashuhudaDSC_0447Mashuhuda.DSC_0449  DSC_0452  DSC_0456 
Dereva wa gari hilo, Michael Augustino akitoa taarifa kwa bosi wake.
DSC_0458 DSC_0463Michael akihojiwa na askari.
MOROGORO: Dereva wa gari dogo la mizigo aina ya lsuzu Carry (Kirikuu) lenye namba za usajiri T 609 CKW, amenusurika kifo baada ya gari hilo alilokuwa akiendesha kuwaka moto katika eneo la Masika katikati ya Mji wa Morogoro, leo 

Wakizungumza na mwanahabari wetu aliyefika eneo la tukio, mashuhuda wa tukio hilo Bernard Joseph na Juma ldd walisema;
“Huyu dereva wa kirikuu alikuwa akitokea eneo la Msamvu (Kituo Kikuu cha Mabasi Yaendayo Mikoani) alipofika hapa Masika jirani na ‘round about’ tulishuhuida gari lake likiwaka moto kwa nyuma na yeye hakuwa na habari aliendelea na safari hivyo boda boda mmoja aliamua kuwasha pikipiki yake na kumkimbilia na kumjulisha tukio hilo ambapo alisimama na kushuhudia gari hilo likiendele kuwaka moto,” walisema mashuhuda hao

Kwa upande wake dereva wa gari hilo aliyejitambulisha kwa jina la Michael Augustino alisema.
“Nashangaa sana huu moto ulikotokea, gari hili injini iko mbele iweje moto utokee huku nyuma ambako hakuna kitu chochote na kama unavyoona sikuwa na mzigo wowote ndani ya gari na washukuru hawa boda boda wa hapa Masika wamenikimbilia na kunipa taarifa za moto huo, vinginevyo ungefika huku mbele kiwa kwenye mwendo wa kasi nahisi milango ingeji-lock na mimi ningeuungua vibaya,”

“Namshukuru Mungu kwa hili”alisema Agostino huku akipiga simu kwa mmiliki wa gari hilo.” Alisema Michael.
Askali wa Kikosi Maalum cha Zima moto, mwenye cheo cha nyota Moja akimhoji dereva wa gari hilo huku wakikagua kifaa maalumu cha kuzima moto kilichokuwa ndani ya  gari hilo.
Picha zote na Dustan Shekidele, Morogoro -GPL
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment