Nitawatumbua MAJIPU Watumishi Wazembe Kabla Sijatumbuliwa -RC Mongella

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema watendaji ambao maeneo yao yataendelea kukithiri kwa vitendo vya uhalifu, migogoro ya ardhi, uharibifu wa mazingira na uchafu atawatumbua majipu.

Akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuhusu kuibuka kwa vitendo vya uvamizi, uporaji na mauaji katika jiji la Mwanza, alisema Serikali haitavumilia kuona watu wasio na hatia wakipoteza maisha na mali zao huku wenye dhamana ya ulinzi wakikaa bila kuchukua hatua.

Mongella alisema: “Sitasubiri nitumbuliwe mimi, nitawatumbua kwanza viongozi na watendaji wazembe kabla sijatumbuliwa.
“Kwa kipindi cha wiki mbili nilichokaa Mwanza kumetokea matukio mawili ya wafanyabiashara ya maduka ya fedha kwa njia ya mtandao kuvamiwa, kuporwa na wengine kuuawa kwa kupigwa risasi, hii haikubaliki na siko tayari kushuhudia vifo vingine."
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment