Mbunge
wa Viti Maalumu, Aysharose Matembe (CCM), amesema vijana na wanawake
mkoani Singida, wameishukuru Serikali kwa kuchagua mkoa huo kuwa
miongoni mwa mikoa 10 ya kwanza itakayonufaika na mgawo wa Sh milioni 50
kila kijiji na kila mtaa.
Matembe
amesema wako tayari kuzitumia kwa uangalifu fedha hizo kwa kuhakikisha
wanaunda vikundi vyenye malengo madhubuti ya kujenga ili wajikwamue
kiuchumi.
Mbunge
huyo jana alisema Singida ni miongoni mwa mikoa yenye rasilimali
nyingi, ikiwemo ardhi yenye rutuba ambayo kwa kiasi kikubwa wananchi
wanaitumia kujishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali yanayochangia
kukua kwa pato la Taifa.
Alisema
amezungumza na wananchi hao ambapo walikiri fedha hizo kuwa na mchango
chanya kwa maendeleo ya mkoa na kaya zao, hivyo kila mtendaji
atakayehusika kwa namna moja au nyingine na fedha hizo, anapaswa kuwa
mwadilifu ili ziwafikie walengwa kwa wakati.
“Kutolewa
kwa hizi fedha ni kama kupatikana kwa maji jangwani kwa vijana na
wanawake wa Singida, kwa nyakati tofauti nimezungumza nao na wananipa
salamu kuishukuru Serikali kwa kuwatambua na kuieleza kwamba wamejipanga
kunufaika nazo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment