Raia
wawili wa China, Ma Jun na Huifang Ma leo wamefikishwa katika Mahakama
ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka mawili likiwamo la kushindwa kutumia
Mashine ya Kodi za Kielektroniki (EFDs) katika biashara zao.
Jun
na Ma, ambao wote ni wafanyabiashara na wakazi wa Mtaa wa Narung’ombe
eneo la Kariakoo wanakabiliwa na kushindwa kutumia mashine za EFDs
pamoja na kushindwa kujisajili katika kodi ya ongezeko la Thamani(Vat)
wakati wakijua kufanya hivyo kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Hata
hivyo, mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Jun hakuwepo mahakamani
hapo kwa madai kuwa yupo nje ya nchi na upande wa mashtaka umeiomba
Mahakama kutoa hati kwa ajili ya kumkamata mshtakiwa huyo.
Akisoma
hati ya mashtaka, mbele ya Hakimu Mkazi Mwanadamizi Mfawidhi wa
mahakama hiyo Said Mkasiwa, Wakili kutoka Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA), Cherubin Chuwa alidai kuwa washtakiwa kwa pamoja walitenda
makossa hayo Machi 23,mwaka huu.
Chuwa
alidai siku hiyo ya tukio, washtakiwa hao ambao wanamiliki Kampuni ya
HM Textile Co Ltd Iliyopo block 54 katika kiwanja namba 6 kilichopo
mtaa wa Agrey eneo la Kariakoo, walishindwa kutumia mashine za EFDs
kwa ajili ya kutoa risiti kwa wateja wao ambao walikuwa wanafanya
manunuzi mbalimbali katika duka hilo ambalo linauza mapazia na nguo
mbalimbali, huku wakijua kuwa ni kosa kisheria.
Mwandesha
Mashtaka huyo aliendelea kudai kuwa, katika shitaka la pili ambalo pia
linawakabili washtakiwa wote, inadaiwa kuwa muda na siku hiyo hiyo
katika duka hilo, washtakiwa walishindwa kujisajili katika kodi ya
ongezeko la Thamani(Vat) wakati wakijua kufanya hivyo kufanya hivyo ni
kinyume cha sheria.
Chuwa
alidai washtakiwa hao walishindwa kujisajili katika Kodi ya Ongezeko la
Thamani(Vat) ambayo ni kinyume cha sheria , na kwamba mashtaka hayo
yamefunguliwa kupitia sheria za TRA.
Hata hivyo mshtakiwa wa pili, Huifang alikiri shtaka la kwanza huku shtaka la pili akikana kuhusika.
Kutokana
na hatua hiyo wakili Chuwa alisema dhamana ya mshtakiwa huyo iko wazi
ambayo ni kuwa na wadhamini wawili kila kutoka taasisi inayotambuliwa
kisheria watasaini bondi ya Sh 3milioni na kuwasilisha mahakamani hati
yake ya kusafiria.
Mshtakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi April 21, mwaka huu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment