‘Kabla Hatujaingia Kwenye Jengo Hili, Tuwe Tunapimwa Kama Tumevuta Marijuana’ -Mbunge Ulega

Bado tunaendelea kuzihesabu stori za Bungeni, najua kuna watu wangu wanakosa nafasi ya kutazama kupitia TV majumbani lakini mimi nahakikisha nakusogezea kila linalonifikia ili na wewe ulipate. Bado Bunge la 11 linapitisha bajeti zinazombwa na Wizara. 

Katika siki mbili za kujadili bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii iliyoomba kutengewa kiasi cha Sh. 135,797,787,000 katika hotuba iliyowasilishwa na  Waziri wake Jumanne Maghembe, Wabunge walipata nafasi pia ya kuchangia ambapo hapa nakukutanisha na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega …  

>>’Wakati mwingine hata mimi nashawishika kufikiria kwamba kabla hatujaingia kwenye jengo hili tuwe tunapimwa kama tumevuta marijuana, katika hali ya kawaida kijana hata kama umepigiwa kura na kuaminiwa na wananchi ukaenda kutukana lazima utakuwa na tatizo kwenye akili yako

Jana yupo mwenzetu mmoja wa kutoka Chama ninachotoka amezungumza mambo ya ajabu sana hapa, unaweza kuona ni kwanamna gani watu hawaelewi ni nani katika nyumba hii ameingia  bila ya Chama kilichomleta. Wote tumezaliwa na vyama vyetu, hii michezo haitaki hasira..!

Watu wa Dar es salaam bado wanatumia nishati ya mkaa, na Serikali inapiga vita matumizi ya mkaa. Nimwambie Waziri nguvu tunayotumia kupiga vita matumizi ya nishati hii, tutumie nguvu hiyohiyo kuhakikisha tunawatafutia nishati mbadala Wananchi hawa

Tunawaambia watumie gesi hata elimu yenyewe ya matumizi ya gesi inafahamika? matumizi ya gesi hayakuanza leo, hata wasomi wenyewe wanaogopa kutumia gesi. Sasa tufanye jitihada za kutoa elimu kabla ya kuwaambia wasitumie wasitumie..!
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment