Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe.
***
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Singida, Simion Mumbee amesimamishwa kazi
baada ya kudaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu watumishi hewa.
Katika
taarifa hiyo, Mumbee anadai watumishi hewa 19 waliogundulika kwenye
halmashauri hiyo hawajaisababishia hasara Serikali jambo linalodaiwa
kuwa si kweli.
Akizungumza
jana kwenye ufunguzi wa kikao cha maendeleo mkoani humo, Mkuu wa Mkoa
wa Singida, Mathew Mtigumwe alisema anamsimamisha kazi mkurugenzi huyo
ili kupisha uchunguzi.
“Nilipotuma
tume kufuatilia suala la watumishi hewa katika Halmashauri ya Wilaya ya
Singida, ilibaini wapo na wameisababishia Serikali hasara ya zaidi ya
Sh125 milioni,” alisema Mtigumwe.
Alisema
taarifa ya Mumbee ililenga kuidanganya Serikali. Mtigumwe alimuagiza
Katibu Tawala wa Mkoa, Dk Angela Lutambi kumuandikia barua ya
kumsimamisha kazi mara moja.
Mtigumwe alisema hana nafasi ya kufanya kazi na watumishi wa aina ya Mumbee.
Wakati
huo huo; Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amemsimamisha kazi
Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Philbert Mtweve kwa
tuhuma za kuwalipa mishahara watumishi hewa wanane na kuisababishia
Serikali hasara ya Sh27 milioni.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment