Waziri Mkuu: Mamlaka ( Halmashauri ) Kusimamia Uwekezaji Wake Ili Zinufaike na Uwekezaji Huo

SERIKALI inaandaa utaratibu utakaowezesha mamlaka husika zikiwemo halmashauri kusimamia zenyewe uwekezaji wake katika maeneo yao ili zinufaike na uwekezaji huo. Imesema imeamua kuchukua hatua hiyo mara baada ya kubaini kupitia mapitio katika eneo la uwekezaji na kubaini mapungufu yaliyopo katika eneo zima la uwekezaji.

Akijibu swali la Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtulia (CUF) bungeni jana, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema utaratibu huo utatoa fursa kwa mamlaka zenyewe kusimamia uwekezaji katika maeneo yake na kunufaika zaidi kuliko sasa.

Katika swali la Mtulia, alitaka kufahamu kwa nini Serikali isiipatie Halmashauri ya Temeke hisa ya angalau asilimia 10 kutokana na uwekezaji wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) kutokana na halmashauri hiyo kutoa ardhi yake yenye thamani ya Sh bilioni 100.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu kitendo cha halmashauri kutegemea tu tozo ya mali na huduma kupitia mradi huu ni uonevu kwani, ardhi ile uliopo mradi wa EPZA ina thamani ya Sh bilioni 100,” alisema.

Akijibu swali hilo, Majaliwa alikiri kuwa kwa sasa Serikali imefungua wigo mkubwa wa uwekezaji ambao unatumia njia mbili kupitia Kituo cha Uwekezaji (TIC) na halmashauri.
Alisema uwekezaji kupitia TIC ambayo inayo benki yake ya ardhi ambayo pia hutolewa na halmashauri husika ambayo yenyewe hunufaika kwa tozo pekee.
Alisema uwekezaji mwingine ni kupitia halmashauri yenyewe kuwa na benki yake ya ardhi na hivyo kuamua kutafuta mwekezaji. Hunufaika kwa kupata tozo na kuwa mwanahisa kupitia mradi husika.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment