WIZARA
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema ina mpango kabambe wa
kujenga barabara za mchepuko katika Manispaa ya Dodoma na nje ya hapo
katika kipindi cha miaka 100 ijayo.
Akizungumza
bungeni Dodoma jana, Naibu Waziri, Edwin Ngonyani alisema utekelezaji
wa ujenzi wa barabara hizo utaanza rasmi pindi fedha zitakapopatikana.
Ngonyani
alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Felister
Bura (CCM) aliyetaka kujua hatua zilizoanza kuchukuliwa hadi sasa na
Serikali kutokana na ahadi aliyoitoa Rais John Magufuli wakati alipokuwa
Waziri wa Ujenzi ya kujenga barabara za mchepuko katika manispaa hiyo.
Aidha,
Bura alitaka kufahamu ni lini ujenzi wa barabara maarufu ya Great North
ambayo hadi sasa ni sehemu ya Tanzania pekee ndio haijakamilika,
itakamilika lini.
Akijibu
maswali hayo, Naibu Waziri huyo alimtaka mbunge huyo asiwe na wasiwasi
kwa kuwa aliyetoa ahadi ya ujenzi wa barabara hizo za mchepuko wakati
akiwa Waziri wa Ujenzi ndiye Rais wa Tanzania.
“Labda
nikujulishe tu hapa nina ramani, tayari kuna mpango kabambe wa kujenga
barabara za mchepuko ndani na nje ya manispaa ya Dodoma katika kipindi
cha miaka 100 ijayo,” alisisitiza.
Alisema katika mpango huo kwa mji wa Dodoma kutakuwa na barabara nane za mchepuko zenye urefu wa kilometa 147.
Akijibu
swali la Barabara ya Great North, Waziri huyo alisema kipande cha
barabara yenye urefu wa kilometa 8.65 eneo la Msalato ni sehemu ya
barabara ya Dodoma-Kondoa-Babati yenye urefu wa kilometa 251. Alisema
barabara hiyo inaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami na imegawanyika
katika sehemu tatu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment