
Azam FC ambao mchezo wa awali uliochezwa Chamazi Dar es Salaam waliibuka na ushindi wa goli 2-1, wamekubali kipigo cha goli 3-0 katika mchezo huo wa marudiano. Kabla ya mchezo huo Azam FC walikuwa wakihitaji ushindi au sare yoyote ya magoli ili waweze kusonga mbele. Magoli ya Esperance yalifungwa na Bguir, Jouini na Errouge.
Baada ya kuondolewa katika michuano kwa klabu ya Azam FC, Tanzania inabakia na muwakilishi mmoja pekee katika michuano ya kimataifa, ambaye ni klabu ya Dar esa Salaam Young Africans ambayo April 20 itacheza mchezo wake wa marudiano na wenyeji wake Al Ahly.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment