BAADA YA KICHAPO KUTOKA COASTAL UNION, KOCHA MAYANJA AIBUKA NA HAYA KWA WACHEZAJI WAKE

KOCHA Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja, amesema wachezaji wake walimuangusha katika mchezo wa Kombe la FA waliopokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Coastal Union juzi.
Kutokana na ushindi huo, Coastal Union imefuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA na kuungana na timu za Yanga, Azam na Mwadui.

Akizungumza baada ya mchezo huo juzi, Mayanja alisema wachezaji wake hawakucheza kama walivyoelekezwa na kuwalaumu Hamisi Kiiza na Juuko Murshid kwa kuchelewa kurudi kutoka Uganda walikokwenda kuitumikia timu yao ya taifa ‘The Cranes’.
“Wachezaji wangu wamepoteza nafasi nyingi, pia wamecheza kwa kiwango duni kisichoridhisha, tunatakiwa tujilaumu sisi wenyewe kwa matokeo tuliyopata,” alisema.

Mayanja alisema Kiiza na Murshid walichelewa kuungana na wenzao mapema kwenye mazoezi, hali iliyosababisha kushindwa kufanya vyema. Kwa upande wake kocha wa Coastal Union, Ally Jangalu alisema timu yake ilifika Dar es Salaam ikiwa imejipanga kuitoa Simba na lengo lao limefanikiwa.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment