Mourinho amekana habari zote zinazo muhusu yeye kuwa hana mkataba wowote wa kuifundisha timu hiyo msimu ujao na kwamba waachene na habari hizo, pia amewaambiwa kuwa Van Gal ni rafiki yake walikuwa wote miaka michache iliyo pita kwa hivo hawezi kuchukua mkataba.
TETESI
Siku kadhaa zilizo pita kulikuwa na tetesi kuwa kocha huyo amesha chukua mkataba wa awali(Pre-Contract) kwa ajili ya kuifundisha Manchester United wakati huo huo kulikuwa na taarifa kuwa Luois Van Gaal imetaarifiwa kuwa atakuwepo msimu ujao na pesa za usajili amepewa.
MTAZAMO
Jose Mourinho mara nyingi hupenda kucheza na akili za watu huenda ameshachukua mkataba lakini kwa kuona thamani na utu wa Van Gaal ambae aliwahi kuwa chini yake hataki aonekane ana fitna ndio maana anaficha ukweli, vile vile vyombo mbali mbali viliwahi kutoa habari kuwa huenda Van Gaal aka staafu baada ya msimu huu kuisha hii pia inatupa matumaini kuwa Jose Mourinho anacheza na hakili za watu yeye ndiye kocha msimu ujao.
HISTORIA
Jose Mourinho (JM) amepata umaarufu alipo ichukua Fc Porto ya Nchini kwake Ureno na kuchukua ubingwa wa Ligi hiyo pamoja na UEFA kama ilivyo kawaida yake akipata mafanikio msimu unao fuata anaondoka baada ya uwekezaji wa Roman Abromovic 2004-2005 katika timu ya Chelsea akamsogeza Stanford Bridge kukinoa kikosi hiko akachukua ubingwa mara mbili wa Epl akatimkia Inter Milan huko nako akachukua UEFA akiwa na Samuel Et’oo baada ya mafanikio aka enda Real Madrid nako kachukua La liga msimu mmoja karudi Chelsea akarudia tena kwa sasa hana timu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment